Kwa namna ya kipekee kabisa, wakazi wa mtaa wa Mivinjeni ndani ya kata ya Buguruni jijini Dar es Salaam, wametoa shukrani zao za dhati kwa kampuni ya ubashiri ya Meridianbet kwa moyo wao wa kujitolea na kugusa maisha yao kupitia msaada wa vyakula na vifaa vya usafi. Kitendo hiki kimeleta faraja kubwa kwa wakazi hawa na kuonyesha kuwa bado kuna taasisi zinazojali jamii kwa vitendo.
Msaada uliopokelewa umejumuisha mahitaji muhimu ya kila siku kama mchele, unga, mafuta ya kupikia, sukari, maharage, sabuni za kufulia pamoja na bidhaa nyingine zinazotumika kwenye matumizi ya kila siku. Msaada huu umekuja kusaidia kupunguza changamoto zinazozikabili baadhi ya familia zilizopo mtaa wa Mivinjeni.
Tunatambua kuwa kaya hizi sio chakula pekee wanachokihitaji, wanahitaji kuonekana, kukumbukwa na kuthaminiwa ingawaje wanapitia changamoto hizi za kiuchumi kwa sasa.
Kwa niaba ya wakazi wote wa mtaa wa Mivinjeni ndani ya kata yetu ya Buguruni, tunamshukuru mwakilishi wa Meridianbet Nancy Ingram pamoja na timu nzima ya kampuni hiyo kwa kututembelea na kutumia muda wao pamoja nasi. Uwepo wao umeacha furaha kubwa mioyoni mwa wananchi na kaya mbalimbali kwa namna moja ama nyingine na umetupa nguvu ya kuendelea kupambana na hali ya maisha bila kukata tamaa.
Tunaziomba taasisi nyingine pamoja na wadau mbalimbali lakini pia na wale wanaohusika na miradi ya kijamii kuendelea kuiga moyo huu wa kusaidia watu wenye uhitaji. Kata ya Buguruni itaendelea kuwa wazi kushirikiana na watu pamoja na kampuni zenye nia ya kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi wetu wanaopitia hali ngumu za kimaisha. Kwa mara nyingine tena, tunasema asanteni Meridianbet kwa kuwa sehemu ya furaha ya wanamivinjeni.
