DC Tarime awafunda viongozi wateule


Na Timothy Itembe Mara.

Mkuu wa wilaya Tarime mkoani Mara Mtemi Msafiri amewataka washindi wateule nafasi ya uwenyekiti wa kijiji, vitongoji na mitaa pamoja na wajumbe wa serikali ya mtaa kwenda kufanyakazi ya kutatua matatizo ya wananchi katika maeneo yao.

Msafiri alisema hayo baada ya wateule hao kuapishwa ndani ya ukumbi wa Chuo cha uwalimu TTC kwa siku  tofauti na Hakimu wa mahakama ya mwanzo, Chana Mahende Chana.

“Kuna changamoto nyingi katika maeneo yenu nendeni mkafanye kazi ya kutatua migogoro ya wananchi, kufanya shuguli za mendeleo pamoja na kudumisha Amani huku mkimsaidia Rais John Pombe Magufuli kazi”alisema Msafiri.

Msafiri aliwataja washindi hao upande wa Tarime vijijini kuwa  kundi mchanganyiko ni watu 902 huku kundi wanawake ni watu 681 na wenyeviti wa vitongoji ni watu 498 na nafasi ya wenyeviti wa vijiji ni watu 88 huku Halmashauri ya Tarime Mjini walioshinda nafasi ya kundi wanawake ni 152 na kundi mchanganyiko ni watu 253 huku wenyeviti wa mitaa ni watu 81 jumla yake ni viongozi 2655.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items