Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema anaunga mkono ongezeko la mauzo ya silaha kutoka ujerumani kwenda katika mataifa ya Afrika ili kupambana na ugaidi katika bara hilo, katika matamshi aliyoyatoa katika bunge la ujerumani leo.
Merkel amesema wakati wa mjadala wa bajeti ya taifa kuwa Ujerumani hazipaswi kuzuiwa katika juhudi zake za kutoa mafunzo kwa majeshi ya kitaifa.
Ameongeza kuwa iwapo Ujerumani inataka kuimarisha usalama na amani katika bara la Afrika, ni lazima majeshi kupatiwa vifaa, akielezea hali ya wasi wasi kuhusu madai ya Ujerumani kuzuwia mauzo ya silaha kwa bara la Afrika.
Jeshi la Ujerumani limekuwa likihusika katika kuwapa mafunzo kwa majeshi ya taifa nchini Mali tangu mwaka 2013 baada ya sehemu kubwa ya mataifa ya Afrika magharibu kuangukia katika udhibiti wa wanamgambo ya kiislamu ambao bado wanaendesha shughuli zao huko.