Klabu ya Chapecoense imeshuka daraja kutoka katika ligi kuu nchini Brazil, siku moja kabla ya kutimiza miaka mitatu tangu timu hiyo kupata ajali ya ndege wakiwa wanaelekea nchini Colombia kwenye fainali ya Copa Sudamericana
Kipigo cha nyumbani cha goli 1-0 kutoka kwa Botafogo walichokipata jana Jumatano, kimewahakikishia kushuka daraja kutoka Serie A na kwenda Serie B zikiwa zimebaki mechi 3 msimu kumalizika.
Wanashuka daraja ikiwa imepita miaka sita tangu wapande kuingia katika ligi hiyo.


