Mamia wamzika mama mzazi wa Naibu Waziri Mabula

Mamia ya wananchi wa jiji la Mwanza na vitngoji vyake wamejitokeza kwa wingi kumzika mama mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula.


Mazishi ya Mama Mzazi wa Dkt Mabula Bi Cecilia Lubala yamefanyika jana kwenye makaburi ya familia yaliyopo kijiji cha Mnyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.


Kabla ya mazishi hayo yaliyohudhuriwa pia na viongozi wa Chama na Serikali kulifanyika ibada maalum ya kumuombea marehemu Cecilia Lubala kwenye Kanika Katoliki Parokia ya Kirumba na baadaye shughuli ya kuaga mwili eneo la Ishungisha wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo William Lukuvi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kilagi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Herry Jemes, Katibu wa UWT Queen Mlozi, Mkuu wa mkoa wa Katavi Anthony Mtaka, Wakuu wa wilaya na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Marehemu Cecilia Lubala alifariki dunia jumamosi iliyopita tarehe 23 Novemba 2019 baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa kwa nyakati tofauti katika hospitali za Muhimbili, Dodoma na Bugando mkoani Mwanza ambako umaiti ulimkuta.