Mawaziri wa uvuvi na sheria nchini Namibia wamejiuzulu baada ya kufichuliwa kwa madai ya kuhusika kwao katika kashfa ya rushwa inayohusisha kampuni kubwa ya uvuvi ya Iceland, Samherji.
Waziri wa uvuvi Bernhard Esau na waziri wa sheria Sacky Shanghala wanadaiwa walitumia vibaya nyadhifa zao kujipatia fedha ili kutoa leseni za uvuvi, ikiwa ni pamoja na kuipatia kampuni ya Samherji, kwa mujibu wa gazeti moja la nchi hiyo, The Namibian.
Samherji imekana madai hayo kuwa ililipa kiasi kikubwa cha fedha kwa maafisa hao katika taifa hilo la kusini mwa Afrika kuweza kukwepa kiasi cha samaki inachostahili kuvua.
Madai hayo yalitolewa Jumanne katika kipindi cha uchunguzi kilichotangazwa katika televisheni nchini Iceland cha Kveikur.
Kipindi hicho cha taarifa za uchunguzi kimenukuu nyaraka , zilizovujishwa katika tovuti ya WikiLeaks zikidai kuwa kampuni ya samherji ililipa mamia ya mamilioni ya krona sarafu ya Iceland kwa wanasiasa na wafanyakazi wa serikali nchini Namibia katika muda wa miaka 10 iliyopita.