Mbunge asikitishwa na ukosefu wa dawa muhimu


Na Hamisi  Abdulrahmani-Masasi

Mbunge wa jimbo la Masasi, Rashidi Chuachua (CCM) amesema kuwa amesikitishwa kuona Hospitali ya mji Masasi Mkoani Mtwara, Mkomaindo inakabiliwa na tatizo la uhaba wa dawa muhimu ikiwemo panado na vidonge vya uzazi wa mpango.

Chuachua aliyasema hayo jana wilayani Masasi wakati alipokuwa akihoji moja ya hoja ilitokana kupitia kwenye taarifa ya kamati ya kudumu ya madiwani ya afya, elimu na maji, iliyowasalishwa na kamati hiyo kwenye kikao cha baraza la Madiwani.

 Alisema kuwa hivi karibuni amepokea malalamiko yanayohusu hospitali ya halmashauri ya mji Masasi juu ya tatizo la ukosefu wa dawa muhimu za binamu.

Chuachua alisema hospitali ya Mkomaindo imekuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa dawa na hata wananchi wanaokwenda kupata matibabu hospilini hapo hukosa dawa hizo.

 Alisema kutokana na tatizo hilo wananchi wanaelezwa kwenda kununua dawa ambazo kwenye hospitali hiyo zinakosekana kununua dawa katika maduka ya watu binafsi.

 Mbunge huyo alisema amesikitishwa na hali iliyopo kwenye hospitali hiyo kwa vile wananchi wanakosa huduma za msingi hivyo kuna kila sababu ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

 Alisema moja ya dawa ambazo zimeonekana kukosekana katika hospitali hiyo ya Mkomaindo ni Panado lakini pia vidonge vya uzazi wa mpango nazo vinakosekana.

"Tunahitaji kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha hizi dawa zinapatikana kwani kwa taarifa niliyonayo katika hospitali hii hili tatizo la dawa ni kubwa kwa wananchi watu," alisema Chuachua

 Aidha,Chuachua aliwataka wataalamu wa sekta ya afya wa Halmashauri hiyo kufanya utafiti juu ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

Akizungumzia kuhusu tatizo hilo la ukosefu wa dawa katika hospitali hiyo ya halmashauri ya mji Masasi, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Gimbana Ntavyo alikiri uwepo wa tatizo hilo.

 Alisema katika mwaka huu mpya wa fedha ulionzia mwezi Julai  halmashauri haijapokea fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa kutoka bohari kuu ya dawa ( MSD)

Alisema Halmashauri kwa sasa imekuwa ikitumia kiasi kidogo cha fedha zake za mapato ya ndani kuagiza dawa lakini hata hiyo mahitaji yamekuwa makubwa..


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia