https://monetag.com/?ref_id=TTIb Meseji nzuri za kumtumia mpenzi wako ili akupenda zaidi | Muungwana BLOG

Meseji nzuri za kumtumia mpenzi wako ili akupenda zaidi

Kila wakati nimekuwa nikisema ya kwamba maneno mazuri yana mchanago mkubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi. Hivyo kila wakati tumia maneno mazuri ili kufanya mpenzi wako akupende daiama.

Zifuatazo ndizo massage nzuri za kumtumia mpenzi wako ili akupende daiam:

1. Wangu kipenzi ninayekuenzi, jua wanitia uchizi na kuninyima usingizi, sijui kama una kizizi au ni mapenzi ndiyo yaninyima huo usingizi, la azizi nimekumiss kichizi, u hali gani mpenzi?

2. Japo umeniuzi sina budi kukupa hizi pongezi, sijui umejifunza wapi mapenzi, hakika kwako mi ni mfungwa wa mapenzi! Nakupenza mpenzi nitunziye langu penzi!

3. Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka kuniacha kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi tambua nahitaji yako hifadhi na niko radhi kukupeleka hadi kwa wangu wazazi, amini kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda.

4. Mpenzi najua u-mbali nami, majaribu ni mengi wapaswa kujihami, nitunzie zangu zabibu wangu tabibu, jitahidi kuwa mvumilivu nitakuja kukutibu, miss u ma luv.

5. Hakika nimepata tabibu, maradhi yangu wajua kuyatibu, napenda jinsi unavyonitibu, huna papara yaani ni taratibu, mpenzi usijemuonyesha mwingine hizo zako zabibu, maswahibu yakatayonisibu hakuna atakayeweza kuyatibu, nakupenda.

6. Nimeamini wewe ni mtalam wajua kunitoa hamu, unipapasapo huhisi kupoteza fahamu, maneno yako matamu hunizidisha hamu, hakika wajua kunikamua, luv u.

7. Kuwa nawe najivunia, mtoto mapenzi wayajua, kiuno, sauti yako tamu mithili ya chiriki wajua hasa kuitumia, mua wangu wajua kuukamua, ukiniacha jua nitaumia, nakupenda usije niacha nitajiua!

8. Dear siku zimekaribia, miaka …… utatimiza katika hii dunia, hakika najivunia kupata mpenzi aliyetulia, hongera kwa wako wazazi kwa kunizalia kipenzi, zawadi yangu toka kwangu ni ahadi ya kulienzi lako penzi. Happy Birthday mpenzi.

9. Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi akupe maisha marefu na kukuepusha na maradhi, pongezi kwa wako wazazi kwa kukuzaa mpenzi, nakupenda la azizi.



10. Siamini kilichotokea, hakika nimekukosea, lakini naapa katu sitorudia, upuuzi niliokufanyia, najua jinsi gani waumia ndiyo maana umeninunia, nisamehe mpenzi nafsi yangu ipate kutulia kwani bila wewe sina thamani katika hii dunia!

11. Namini utakuwa umerejea kwenye yako makazi na umechoka na kazi mpenzi, badili yako mavazi, bafuni ingia upate maji kujimwagia, nakupenda la azizi, pole sana na kazi!

12. Giza limeingia simuoni wakunikumbatia niko kama kinda la njiwa na zaidi ya mshitakiwa mwenye hatiya, sjiui wapi joto kwa kwakulipatia na wajua kipupwe kimewadia, uko wapi my dear?