Mikoa inayoongoza kwa Bangi yatajwa na Serikali


Serikali imesema licha ya kufanikiwa katika jitihada kubwa kwenye mapambano ya dawa za kulevya, bangi bado ni tatizo kubwa hasa katika mikoa ya Mara, Tanga, Morogoro, Arusha, Kagera na Ruvuma.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema lengo la kutoa taarifa hiyo kwa jamii, ni kuwafahamisha wananchi hali ya dawa za kulevya hapa nchini na jitihada za Serikali katika kupambana na tatizo hilo.

"Licha ya jitihada hizo lakini Bangi bado ni tatizo kubwa hapa nchini, na mikoa ambayo imeonekana kuathirika zaidi na kilimo cha Bangi ni pamoja Mara, Tanga, Morogoro, Arusha, Kagera na Ruvuma," amesema.

Ameendelea kwa kusema, "Pia Milungi imeendelea kutumiwa na watu wa rika mbalimbali kwa kipindi cha mwaka 2018, juhudi za za Vyombo vya Dola vimefanikiwa ukamataji wa tani 24.3 za Bangi na watuhumiwa 10,061, na tani nane 8.97 za mirungi na watuhumiwa 1,186,".