Watu wapatao sita wamepoteza maisha na wengine 15 kujeruhiwa hapo jana kufuatia moto uliosababishwa na mlipuko wa bomba la mafuta lililokuwa linavuja katika jimbo la Beheira nchini Misri.
Kwa mujibu wa Wizara ya Nishati nchini humo,uvujaji huo ulitokana na shimo lililokuwa kwenye bomba la mafuta liliotokea baada ya wizi wa petroli kutofua dafu.
Maafisa wa Beheira walisema kuwa watu hao walikutana na kifo walipokuwa wakikimbilia eneo hilo lenye bomba la mafuta.
Naye Katibu Mkuu wa jimbo la Beheira Hazem al-Ashmouny alipokuwa akitoa salamu zake za rambirambi alikieleza kituo cha Egypt State TV kuwa moto huo uliweza kudhibitiwa haraka mara moja.
