'Mungu wa Kichina apelekwa Thailand'


Mashua iliyobeba sanamu ya Mazu ambaye 'mungu' wa zamani wa bahari wa China, ilisafiri hapo jana asubuhi kutoka Kisiwa cha Meizhou katika mji wa Putian, Mkoa wa mashariki wa China, ikiashiria kuanza kwa safari ya siku saba ya Mazu kwenda Thailand.

Wakipiga ngoma, maelfu ya wenyeji walipuga foleni kwa hiari kando ya barabara ili kuona sanamu yao ikielekea nchi ya kusini mashariki mwa Asia.

Kama ilivyopangwa, Mazu aliondoka kisiwa cha mji wa pwani wa Xiamen kwa kivuko na basi. Katika Xiamen, atakaa usiku mmoja kabla ya kwenda Bangkok.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items