Mwanamuziki Prezzo afunguka tuhuma za kubakwa na wanawake watatu hadi kulazwa Hospitali


Msanii wa Kenya Prezzo amekanusha taarifa za kukimbizwa Hospitali na kulazwa baada ya Kubakwa na wasichana watatu hotelini.

Vyanzo vya habari nchini Kenya viliandika kwamba Prezzo amelazwa katika hospitali ya Karen mara baada ya kuchanganyiwa dawa za kulevya aina ya Cocaine na Viagra na kulewa kisha Kubakwa na wasichana watatu katika chumba kimoja cha hoteli.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na yupo salama kabisa.

Ametangaza pia kuwachukulia hatua wote ambao wamekuwa wakimchafua kwa kuandika taarifa za kupotosha kuhusu yeye na muziki wake kwa ujumla.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia