Aliyekuwa kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema anarudi Tanzania kufuata malimbikizo ya madeni yake kwa uongozi wa klabu hiyo.
Zahera alifungashiwa virago vyake baada ya kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo ambapo nafasi yake inakaimiwa na Bonface Mkwasa.
Zahera amesema hakuna mahala aliposaini barua ya kutimuliwa Yanga na hajalipwa malimbikizo ya madai yake hivyo anarudi kufuata.
Wakati hayo yakijiri naye kocha wa Simba, Patrick Aussems ameendelea kutumikia adhabu yake huku kikosi chake kikijifua kwenye Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam. Mazoezi hayo yamefanywa chini ya msaidizi wake, Denis Kitambi ambaye alijikita zaidi katika kuwapa wachezaji mazoezi ya kumiliki mpira na kufunga.
