Ng'ombe wafungwa vifaa machoni ili kuwatuliza na kujiona katika mazingira mazuri


Wakulima nchini Urusi wameanza kuwafunga ng'ombe wao vifaa vya 'virtual reality' ili kuwafanya wawe watulivu kwa kujiona wapo katika mazingira mazuri, na waongeze maziwa.

Matokeo ya awali yameonesha ng'ombe walionekana wenye furaha zaidi kuliko walivyokuwa bila wakitazama mazingira halisi.

Bado haijaelezwa kuwa kama kwa namna yoyote vifaa hivyo vimewezesha ng'ombe hao kutoa maziwa zaidi ukilinganisha na kiasi cha maziwa walichokuwa wanatoa hapo awali.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items