RC Kagera avibana vyama vya Ushirika


Mkuu wa mkoa Kagera Brig. Jen Marco E Gaguti amevitaka vyama vya ushirika Kagera KCU na KDCU kumuonyesha ni jinsi gani mali zinazomilikiwa na vyma hivyo zitakavyotumika kuleta tija katika zao la kahawa na kuleta tija kwa mkulima wa zao hilo na kupunguza gharama kwa mwendeshaji wa miradi hiyo inayomilikiwa na vyama hivyo.


RC Gaguti amesema amesema kuwa atakutana na vyama hivyo mwezi wa kumi na mbili ili vyama hivyo vimuonyeshe mali zinazomilikiwa na vyama hivyo lengo likiwa ni kuona jinsi gani vyama hivyo vinarudisha faida kwa mkulima na kujiendesha kwa tija.

“Tarehe 07/12/2019 nitakutana na KCU na tarehe 08/12/2019 nitakutana na KDCU ili mnionyeshe aseti mlizo nazo na mpango mkakati wa hizo aseti wa kuongeza thamani na kupunguza gharama za uendeshaji za vyama vyetu vikuu vya ushirika kwahiyo nawapa mwezi huu mmoja nione,” Amesema RC Gaguti.

Aidha RC Gaguti amewataka watu na taasisi zilizokopa katika bank ya wakulima Kagera na kusababishwa Bank hiyo kufungwa kurudisha pesa wanazodaiwa ndani ya siku nne na kujisalimisha katika kamati ya usalama ya mkoa na atakayeshindwa kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria. “hakuna taarifa niliyowahi kuipata mezani kwangu kwa mwaka wowote wa fedha ikionesha mmekusanya kiasi gani cha fedha kwa mwaka wowote,kwa maana hiyo hizi asets hazina maana yoyote katika ushirika wetu na kilimo cha kahawa.”

Mbali na hayo RC Gaguti ametembelea kiwanda cha kukoboa na kusaga kahawa kinachomilikiwa na BUKOP na COFFE TREE HOTEL ili kujionea uendeshaji wa miradi hiyo.