Uganda: Padri akabiliwa na kesi ya mauaji


Padri wa wa Kanisa Katoliki katika dayosisi ya Kiyinda Mityana nchini Uganda, Lawrence Muduse na wenzake wamewekwa rumande kwa tuhuma za kumuua Muhammad Kimbugwe mkazi wa kijiji cha Minaana.

Washtakiwa wengine ni John Kulumba Mkubwa, John Kulumba Mdogo, Jane Nankabirwa Kulumba, Ibrahim Muyingo, Robert Ssenyange na Fred Kayongo.

Ripoti inaeleza kuwa, Padri huyo pamoja na wenzake walipokuwa katika kijiji cha Minaana siku ya Agosti 7 mwaka huu walimuua Bwana Muhammad wakati akiwa anasambaza barua kwa wapangaji wake katika ardhi yake iliyopo kijijini hapo.

Aidha, watu hao wamewekwa rumande mpaka siku ya Desemba 4 mwaka huu itakaposomwa mbele ya Mahakama Kuu ya Halmashauri ya wilaya ya Mityana.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items