Ugiriki yakumbwa na tetemeko la ardhi

Tetemeko la ardhi enye ukubwa wa 6.1 limetokea kusini mwa Peninsula nchini Ugiriki.

Kulingana na ripoti yaa awali, Taasisi yinayohusika na matetemeko ya ardhi nchini humo ilitangaza kwamba tetemeko hilo lilitokea saa 09.23 eneo hilo, kwa kina cha kilomita 20 baharini kati ya kisiwa cha Kythera na kisiwa cha Krete, kusini mwa Peloponnese.

Vyombo vya habari vya eneo hilo vimetangaza kwamba tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.1 lilisikika sana kutoka mji mkuu wa Athene, hadi kisiwa cha Krete, umbali wa kilomita 258.

Hata hivyo wanasayansi wamebaini kuwa tetemeko hilo halina uhusiano wowote na tetemeko lililotokea jana huko Albania.

Hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu kupoteza maisha au uharibifu wa mali.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items