Ujenzi wa mabanda soko la Ferry wamkuna Meya wa Ilala

Katika kuhakikisha serikali inatengeneza mazingira rafiki kwa kila mwananchi kuelekea uchumi wa kati hii leo Mstahiki Meya wa Manisipaa ya Ilala Omary Kumbilamoto ameridhishwa na kasi ujenzi wa mabanda ya mama lishe na wavuvi katika soko la kimataifa la Ferry jijini Dare s salaam.


Kumbilamoto amesema ujenzi umefikia asilimia 99 Mara baada ya kufanya ziara na kujiridhisha kuwa zile fedha milioni 20 alizozitoa kwa ajili ya kuanza ujenzi huo na badae manispaa ya ilala kuongeza zaidi ya milioni 16 zimeendana na thamani halisi ya majengo.


Aidha Kumbilamoto amesema kwa mwaka soko la samaki Ferry huingizia Manispaa ya Ilala kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja na kwamba kama manispaa wanatarajia kujenga soko jingine jipya ili kuzidi kuongeza ufanisi kwa wafanyabiashara hao.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items