Umoja wa UIaya watumai Marekani itatafakari kuhusu uamuzi wa kujiondoa mkataba wa Paris

Umoja wa UIaya umeelezea kusikitishwa kwake na hatua ya serikali ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya Paris ya mazingira na ikaelezea matumaini kuwa nchi hiyo ambayo ni moja ya watoaji wakubwa wa hewa inayochafua mazingira itaubatilisha uamuzi huo na kujiunga tena.

 Msemaji wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Mina Andreeva amesema kuwa mkataba huo wa kimataifa uliotiwa saini mwaka wa 2015 unabaki kuwa makubaliano muhimu kabisa ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na akasisitiza kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kupambana na mabadilkiko ya tabia nchi chini ya mfumo huo wa kisheria.

 Licha ya kuondoka kwa Marekani, Andreeva ameongeza kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kufanya kazi na mashirika mbalimbali ya Marekani na wadau ambao wanadhamiria kuutekeleza mkataba huo
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items