Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu awashukuru Wahisani kutoka nchi ya Korea kwa msaada katika Sekta ya Afya nchini.
Amesema, vituo kadhaa vya kutolea huduma za afya hapa nchini vilivyopo katika maeneo ya Mbagala, Temeke, Chanika, Sinza na maeneo mengine ukiacha Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mlonganzila jijini Dar es Salaam vimejengwa na kufanyiwa ukarabati mkubwa kwa ufadhili wa wahisani kutoka nchi za Korea.
Waziri Ummy amesema haya, alipokutana na wahisani mbalimbali kutoka nchini Korea Kusini katika Ofisi za Wizara NHIF Jijini Dodoma.


