Dec 4, 2019

Frederick Sumaye afunguka kugombea Urais 2020 kupitia ACT Wazalendo


Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema taarifa za yeye kugombea Urais 2020 kupitia Chama cha ACT Wazalendo hazina ukweli wowote.

Ameeleza hayo leo mbele ya Wanahabari alipokuwa akieleza sababu ya kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

“Kuhusu kwamba nina mpango wa kujiunga na Chama cha ACT ili nigombee Urais mwakani hizo taarifa hazina ukweli, nimeondoka CHADEMA ila sijajijunga na Chama chochote” amesema Sumaye.

Aliendelea kwa kusema, “Labda kwa kitendo hiki cha kuondoka CHADEMA Mke wangu na Wanangu watanivalisha Taji kwa kuwaondolea adha walizokuwa wanapambana nazo kwa mimi kuwa Upinzani, jambo jema tuheshimiane na tuheshimu utu wa Mtu” .

Sumaye alikuwa waziri mkuu mwaka 1995 hadi 2005 amesema hayo takribani siku nne tangu alipopigiwa kura 48 za hapana kati ya 76 katika uchaguzi wa uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger