Rais wa Namibia, Hage Geingob amechaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo akipata asilimia 56.6 ya kura zote dhidi ya mpinzani wake Panduleni Itula aliyepata asilimia 29.4.
Ushindi wa Geingob umeshuka kutoka asilimia 87 alizopata aliposhinda mwaka 2014.