Loading...

12/04/2019

Victor Wanyama anunua basi kwa ajili ya timu za kitongoji alichozaliwa


Kiungo wa klabu ya Tottenham Victor Wanyama amezinunulia klabu za nyumbani kwao Muthurwa, Kenya basi ambalo watalitumia katika shughuli za usafiri.
 
Wanyama alizaliwa na kukulia Muthurwa, Kenya na kuanza soka lake katika klabu ya Country Bus iliyopo Muthurwa.
 
Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Kenya kupitia Victor Wanyama Foundation amenunua basi hilo la siti 40 jijini London, Uingereza na kulisafirisha mpaka Muthurwa. Basi hilo litatumiwa na Country Bus FC na Muthurwa Boxing Club
 
Akiongea na N“Siwezi kukimbia ukweli kwamba nilizaliwa na kukulia Muthurwa na Country Bus FC walikuza kipaji changu. Ninafuraha kurudisha katika timu na nina hakika huu utakuwa mwanzo wa timu kupanda juu.”
.
“Muthurwa inafahamika pia kwa kuzalisha mabondia wazuri na hii hii kwa heshima ya Boxing Club. Basi hili pia litawasaidia (mabondia) wakati wowote watakapokuwa wanasafiri kwa ajili ya mechi au kazi zozote watakazokuwa nazo.”
.
Wanyama,28, pia ametangaza kupitia Victor Wanyama Foundation kuwa ametoa ofa ya ufadhili (Scholarship) kwa wanafunzi wawili (wakike na wakiume) waliopata maksi 400 na zaidi katika mtihani wa Taifa wa elimu ya Msingi mwaka 2019.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger