Na Amiri kilagalila-Njombe
Imeelezwa kuwa ajali nyingi za bodaboda ambazo zimejitokeza mwaka 2019 katika halmashauri ya mji wa makambako mkoani Njombe zimesababishwa na uzembe wa madereva kutokana na kuendesha kwa mwendo mkali.
Mratibu wa elimu ya usalama barabarani wilaya ya kipolisi Makambako kitengo cha usalama barabarani Bryson Kambo wakati akizungumza na madereva bodaboda,amesema kitendo cha kutembea kwa spidi kubwa na kutokuheshimu alama za barabarani ndiyo sababu kubwa zinazopelekea kutokea kwa ajali hizo.
“baadhi yetu tumekuwa tukiendesha piki piki bila kujali upo mazingira gani,uwe unakatisha sokoni unaendesha kwa mwendokasi,upo ndani ya stendi unaendesha kwa mwendokasi na kuna wengine kati kati ya mji wanaendesha kwa mwendokasi na kuna wengine hata piki piki zao hazina bima naomba haya yarekebishwe”alisema Bryson Kambo
Kambo amesema kwa mwaka 2020 madereva wote wanatakiwa kuzingatia sheria zote za uendeshaji wa vyombo vya moto hususani kuvaa kofia ngumu na kupakia abiria wanao takiwa kwa kuwa jeshi hilo limejipanga kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaobainika na makosa.
“2020 tutanyooka sheria haitapinda hata kidogo haitaonea huruma mtu”amesema Kambo
Kwa upande wa madereva bodaboda mjini Makambako wamesema watahakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani na wameliomba jeshi hilo kuendelea kutoa elimu ili wazidi kukumbushana.
