China na Marekani zinatarajiwa kutia saini makubaliano ya awali ya biashara ambayo yanalenga kuongeza kwa kiasi kikubwa, ununuzi wa China wa bidhaa zaidi kutoka Marekani.
Vita vya kibiashara kati ya nchi hizo vinatarajiwa kuingia katika awamu ya utulivu leo wakati rais Donald Trump na makamu wa rais wa China Liu He watakapotia saini makubaliano ya China kuongeza ununuzi wa bidhaa za kilimo, nishati na huduma.
Makubaliano hayo ya awamu ya kwanza yanafikisha mwisho miezi 18 ya mzozo wa ushuru kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani, ambao umeathiri mamia ya mabilioni ya bidhaa, masoko ya fedha, kuharibu njia za kusambaza bidhaa pamoja na kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi duniani.
Trump na Liu wanatarajiwa kutia saini waraka wenye kurasa 86, katika tukio litakalofanyika katika Ikulu ya Marekani ya White House mbele ya zaidi ya wageni waalikwa 200 kutoka katika duru za makampuni, serikali na wanadiplomasia.