Diwani aishauri Halmashauri kununua mitambo ya kuchimba visima

Na Timothy Itembe Mara.


Diwani viti maalumu kata ya Matongo kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema,Filomena Tontora ameishauri halmashauri ya Tarime juu ya kununua mitambo ya kuchimbia visima vya maji na kuondokana na watu kunywa maji yenye sumu hususani wakazi wa Nyamongo.

Tontora alisema kuwa halmashauri imekuwa ikitumia fedha nyingi kwa wakandarasi huku baadhi ya Wakandarasi hao wakiwakwamisha katika shuguli nyingi za kimaendeleo ya Wanachi  kutotekelezwa miradi kwa wakati  kwa madai mbalimbali ambayo  mengine hayana  sababu za misngi.

“Mimi nishauri halmashauri yangu badala ya kutegemea Wakandarasi miaka yote ambao  wanapewa tenda ya kutekeleza miradi ya halmashauri na baadhi yao wakishindwa kutekeleza kwa wakati huku wakitusumbua,na wakandarasi wengine sisi madiwani tukifuatilia miradi iliyokuja ndani ya kata zetu wanatuita kuwa sisi ni mambumbu  hatujui lolote na hatuwezi kupewa BOQ mikataba ya makubaliano ya utekelezaji wa mradi ninaomba halmashauri sisi ili tuondokane na kero hiyo tununue  mitambo yetu ya kuchimba visima vya maji”alisema Tontora.

Tontora aliongeza kuwa halmashauri isiishie kununua mitambo ya kuchimba visima vya maji tu iende mbali na kununua  na kumiliki mitambo ya kulima barabara kwasababu  wakandarasi wengi wanaopewa kulima Barabara wanasumbua sana.

Kwa upande wake Diwani kata ya Bumera kupitia Chama cha mapinduzi Deogratius Ndege alisema kuwa yeye binafsi anawasiwasi kubwa kuwa  fedha zinazotolewa na Serikali kuja halmashauri  juu ya utekelezaji wa miradi kwa jamii huwenda zinatumika vibaya hazitumiki  vizuri inawezekana kuna wapiga dili katika hiyo miradi.

 Naye Slyevanus Gwiboha  kaimu mkurugenzi wa kikao cha jana ambacho kilifanyika katika ukumbi wa Shule ya sekondari JK Nyerere Nyamwaga alisema kuwa halmashauri yake imetenga fedha kwa ajili  ya manunuzi ya mitambo ya kuchimba visima vya maji ambapo  mchakato wake  umepelekwa kwa Wakala wa manunuzi wa serikali.