Iran yatoa onyo kwa majeshi ya Ulaya

Rais wa Iran amesema leo kuwa vikosi vya majeshi ya Ulaya katika mashariki ya kati vinaweza kuwa katika hatari , iwapo mataifa yao yatajiunga na kampeni ya Marekani yakuweka mbinyo mkubwa dhidi ya taifa hilo la Jamhuri ya Kiislamu iliyosababisha mivutano ya kijeshi mapema mwezi huu.

 Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimejaribu kwa miezi kadhaa kulinda makubaliano ya kinyuklia ya mwaka 2015 baada ya rais Donald Trump wa Marekani kuitoa nchi hiyo mwaka 2018.

Lakini jana, Umoja wa Ulaya ulianzisha mfumo wa kutatua mizozo kujaribu kuirejesha Iran katika utekelezaji baada ya Iran kuanza kukiuka baadhi ya masharti ya makubaliano kuanzia katikati ya mwaka uliopita.

Iran imesema haitafungwa na makubaliano hayo kwa kuwa Marekani imerejesha vikwazo vinavyoumiza uchumi wa nchi hiyo.

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yana maelfu ya wanajeshi nchini Afghanistan, Iraq na kwingineko katika mashariki ya kati, ambako yanafanyakazi kwa kiasi kikubwa pamoja na majeshi ya Marekani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items