Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wanamshikilia Kijana Seif Machano mwenye miaka 28 kwa tuhuma za kumteka Mtalii ambaye ni Raia wa Marekani Sheiley Moris na kuiba kila kitu chake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Awadhi Juma amesema Mtuhumiwa akiwa na wenzake ambao hawajapatikana walimteka Raia huyo wa Marekani kwa kutumia Noah na kisha kumtaka atoe kila kitu ili kuokoa maisha yake.
"Tunamshikilia Seif tulimkuta na ATM card za Mmarekani na vingine na wenzake watapatikana kisha wote watafikishwa Mahakamani"