Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido ameitisha maandamano ya siku tatu dhidi ya Rais Nicolas Maduro masaa kadhaa baada ya kula kiapo cha awamu nyingine ya kuwa spika wa bunge la nchi hiyo.
Guaido ambaye awali alizuiwa kuingia bungeni na walinzi wa serikali huku mpinzani wake akiwa amerithi wadhifa huo amesema maandamano hayo yatafanyika Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi.
Bunge la taifa la Venezuela ndiyo muhimili pekee wa serikali unaodhibitiwa na upinzani. Wabunge waliimba wimbo wa taifa na ghafla umeme ulikatwa hali iliyowalazimu kutumia tochi za simu zao za mkononi.
Guaido hatimaye alikula kiapo cha kuliongoza bunge kwa kipindi kingine. Rais Maduro amesema hatua ya kuapishwa Guaido ni sawa na mchezo wa kuigiza na amemshutumu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo kwa kumuunga mkono.