Kiungo wa Chelsea atimkia Aston Villa

Kiungo wa klabu ya Chelsea Danny Drinkwater, amekamilisha usajili wake wa mkopo kwenda klabu ya Aston Villa ambapo ataitumikia klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu.

Drinkwater aliutumia nusu ya msimu huu akicheza kwa mkopo kwenye klabu ya Burnley, lakini mkataba huo wa mkopo ulimalizika Januari 6 na sasa anajiunga na Villa.