Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo ametoa siku 7 kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kuvunja mkataba na mkandarasi wa kampuni ya Juniour Construction anayekarabati barabara ya Naiyobi mpaka eneo la View Point baada ya kutoridhishwa na kasi ya ujenzi ya mkandarasi huyo licha ya kuongezewa miezi mitano bado barabara hiyo haipitiki.
Akizungumza katika ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi wa barabara ,wakati akikagua barabara hiyo iliyotengewa shilingi bilioni 1.39 mkoani Arusha ameeleza kusikitishwa na Mkandarasi huyo licha ya umuhimu wa barabara hiyo kwa watalii wanaotembelea Ngorongoro kwani jambo hilo ni hujuma kwa taifa .
Mrisho Gambo amesema kuwa Bodi ya NCAA ikae na kufanya maamuzi ya kuvunja mkataba kwa kufuata taratibu zote kwani barabara hiyo ya kilomita 78 imekarabatiwa kilomita 14 pekee na hizo 14 haziko katika hali ya kuridhisha hivyo hatua zichukuliwe dhidi yake.
Aidha ameitaka mamlaka hiyo kuangalia namna ambavyo mkandarasi huyo alipatikana kwani amenekana kutokua na sifa kutokana na utendaji wake mbovu unaokwamisha miradi ya barabara .
Kaimu Kamishna Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Assangye Bangu amesema kuwa wamepokea agizo hilo na watalitekeleza kwa haraka ili kutatua changamoto ya miundombinu mibovu na kuhakikisha barabara zinapitika.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Steven akieleza kuwa kitendo kinachofanywa na Mkandarasi huyo ni kuhujumu utekelezaji wa Ilani ya CCM na hakitafumbiwa macho hivyo anapaswa kuwajibishwa ndani ya siku 7 zilizotolewa.