Na John Walter, Siha Kilimanjaro
Wafugaji wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro wameiomba serikali kuwaongezea maeneo ya Malisho ili kuondoa migogoro baina yao na wakulima kutokana na ongezeko kubwa la mifugo hadi kukosa maeneo ya kutosha ya malisho.
Wametoa ombi hilo Hayo kwenye uzinduzi wa zoezi la kuogesha mifugo linalosimamiwa na Wizara ya mifugo katika kanda ya kaskazini, ambapo wafugaji hao wamesema kumekuwepo ongezeko la mifugo hali ambayo inaweza kupelekea kurejesha migogoro ya nyuma kati ya wakulima na wafugaji.
Nae daktari wa mifugo wilaya ya siha Barnabasi Mmbwambo amesema kuwa zoezi la kudhibiti vifo hususani kwa ndama zilizokuwa zinakufa kabla ya kukua kutokana na magonjwa yatokanayo na kushambuliwa na kupe wameweza kulidhibiti kwa kiasi kikubwa lakini kwasasa changamoto ni eneo la malisho kwa mifugo.
Eneo ambalo wafugaji hawa wanalitumia ni hekari 2,000 wakati wilaya ya Siha ikitajwa kuwa na mifugo zaidi ya laki Moja.