Agrrey Moris apigwa faini kisa waandishi wa habari

Nahodha wa Azam FC, Agrrey Moris amepigwa faini ya kiasi cha laki mbili  (Tsh. 200,000/=) kwa kosa la kugoma kuongea na  Waandishi wa habari  mara baada ya mchezo wa ligi kati ya Azam FC (1-1) kumalizika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari  10, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;

Mechi namba 189:Azam Fc 1 vs Tanzania Prisons Fc 1

Morris amepigwa faini ya kiasi cha Tsh 200,000/=(Laki Mbili) kwa kosa la kugoma kuongea na  waandishi wa habari  mara baada ya mchezo kumalizika katika mechi iliyochezwa Februari 05,2020 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Adhabu hii imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia