China imekanusha leo kujihusisha kwa vyovyote katika wizi wa mitandao, kufuatia hatua ya Marekani kuwashitaki wanajeshi wanne wa Kichina kwa tuhuma za kuhusika na udukuzi mkubwa wa mwaka wa 2017 wa shirika lake linaloripoti kuhusu madeni la Equifax.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Geng Shuang amesema serikali ya China na jeshi hawajihusishi kamwe na shughuli za wizi wa kibiashara kupitia mtandao wa intaneti.
Wizara ya sheria ya Marekani inawatuhumu wanajeshi hao kwa kuiba taarifa binafsi za Wamarekani wanaokadiriwa kufikia milioni 145, wakikusanya majina, mahali wanapoishi, namba za mafao ya kijamii na leseni za kuendesha magari pamoja na data nyingine zilizohifadhiwa katika kampuni hiyo ya hifadhi ya data.
Udukuzi huo unaathiri hadhi ya kampuni hiyo na inaelezea kuhusu China inavyofanya juhudi katika wizi wa data pamoja na mbinu za kisasa zaidi za kukusanya taarifa za kijasusi.
Kesi hiyo ni ya hivi karibuni kabisa kwa Marekani kuwashutumu wadukuzi wa China kwa kuingilia data za makampuni ya Marekani.