Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa ametembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu waenezao Malaria (Tanzania Biotech product limited – TBPL) kilichopo chini Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kilianzishwa kwa ushirikiano wa nchi ya Cuba baada ya nchi hiyo kukubaliana kuipatia Tanzania teknologia ya kuzalisha viuadudu.
“Hatuhitaji kuongeza jengo wala mitambo mingine na nikatoa magizo kwamba ndugu zetu wa Cuba kwa sababu nyie ndo mnatoa teknolojia, boresheni ili tuanze kutengeneza viuatilifu kwa ajili pamba, lakini mpaka sasa hakijafanyika kitu” Bashungwa
“Maana pamba peke yake nchini kila msimu tunatumia kiasi kisichopungua Bilioni 40 kuagiza viuatilifu kutoka nje na kwenye korosho Bilioni 30, kwa hivyo tu wiwili tunatumia Bilioni 70 kila msimu kuagiza kutoka nje, zingekuwa zinakuja hapa kiwanda kinafanya hiyo kazi maana soko lipo” Bashungwa
“Kiwanda hiki NDC wewe una ubia 100% na hawa watu wanatupa teknologia tu, kwa vile tumeshaona watu hawa hawatufai, Katibu Mkuu inabidi tuwasiliane na Mambo ya Nje hawa watu hawatufai, hii timu iondoke walete timu nyingine ambayo itashirikiana na serikali kuendesha kiwanda” Bashungwa
