Iran: Watu 6 wafariki kutokana na virusi vya corona

Watu 6  miongoni mwa watu 28 walioripotiwa kupimwa na kukutwa na virusi vya Corona nchini Iran wamefariki.

Mamlaka  nchini Iran imefahamisha kuwa  watu 6 miongoni mwa watu 28 waliopimwa na kukutwa na virusi vya corona wamefariki.

Vipimo alivyofanyiwa  muathirika  wa mwisho vilionesha kuwa licha ya kuwa alikuwa na virusi vya corona alikuwa okisumbuliwa na maradhi ya moyo.

Maafa hayo  yametokea  katika mji wa Arak.
Kwa upande wake, wizara ya afya nchini China imefahamisha kuwa idadi ya maafa kutokana na virusi vya corona  imepungua kwa kiasi kikubwa.

Hadi kufikia  Jumamosi Februari 22 watu ambao wamekwishafariki kutokana na  virusi hivyo vya corona imefikia watu 2345.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items