Jifunze namna ya kushukuru kwa yale mazuri unayopata

Kuna wajenzi wawili walikuwa wakijenga ghorofa. Mmoja alikuwa juu na kibarua alikuwa chini. Sasa kuna muda yule mjenzi alihitaji kuwasiliana na kibarua chini.. lakini kibarua alikuwa busy mbali naye.. na alipojaribu kumuita hakusikia maana walikuwa mbali mbali.

Yule mjenzi akaamua kumrushia noti ya 5000 ili ashtuke na kuangalia nani anarusha?
Yule kibarua akaokota hela akaweka mfukoni na kuendelea na yake
Mjenzi akaamua kurusha hela kubwa zaidi.. labda atatia akili aangalie juu.
Ndio kwanza kibarua akachukua hela akaweka mfukoni akaendelea na yake.

Ndipo mjenzi akaamua kuchukua jiwe pale alipo katika ujenzi wake.. akamrushia.. likamgonga... kwa maumivu akashtuka na kuangalia nani anampiga?

Ndipo mjenzi akapata mawasiliano naye.

Je mara ngapi MUNGU anatupa baraka zake.. zawadi mbali mbali.. zinazovutia.. ndio kwanza  tunachukua na kuweka mfukoni na kuendelea.. bila hata kuinua macho kumshukuru.. au kuwasiliana naye Zaidi.

Sometimes ili tushtuke na kuinua macho..  Mungu anatupa jiwe ili tugeuke tuutambue uwepo wake na kuongea naye. Anaachilia magonjwa sometimes ili tuwasiliane...

Unatakiwa kuelewa saa ya amani ndio ya kuomba. Saa ya afya ndio ya kuomba Mungu awe nawe.

Saa ya mafanikio ndio saa ya kuwasiliana na aliyekupa.  Ili akupe zaidi. Usisubiri viondoke ndio uanze kuuliza why?