Makocha wa Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons wafunguka baada ya kutoka suluhu



Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Timu ya Tanzania Prisons leo imeshindwa kuondoka na pointi zote tatu na kuambulia pointi moja baada ya kutoka suluhu na timu ya Mtibwa Sugar ya Mjini Morogoro katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.

Mara baada ya mchezo huo Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema makosa ya washambuliaji wake ndio yaliyowafelisha kuondoka na pointi zote tatu kwa kukosa nafasi nyingi ambazo walizipata.

"Bado hatujakata tamaa timu inacheza vizuri kwa mfano leo makosa ya washambuliaji ndio  yaliyotukosesha ushindi lakini tutazidi Kupambana kuhakikisha michezo ijayo tunarekebisha makosa hayo" amesema Katwila.

Kwa upande wake Kocha wa Tanzania Prisons Adolf Richard amesema anashukuru hata kwa pointi hiyo moja waliyopata amesema bado Kuna mechi nyingi makosa madogo madogo hayo watayalekebisha kuhakikisha timu inaendelea kushinda.

Aidha kuhusu kucheza vizuri wanapocheza na timu za Simba na Yanga, amesema sio kwamba huwa wanakamia mchezo bali Michezo hiyo ilichezwa katika uwanja mzuri ambao unaruhusu kila timu kucheza.

" Sio kama tunakamia hizi mechi za Simba na Yanga tumecheza katika uwanja mzuri, ukiangalia uwanja wa taifa ni mkubwa na unapichi nzuri (sehemu ya kuchezea) na ukiangalia uwanja wa Uhuru una nyasi bandia kila mchezaji anacheza kwa kiwango chake" amesema Adolf Richard.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items