Na John Walter-Babati-Manyara
Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Paulina Gekul (CCM) amesema tangu ahamie chama cha Mapinduzi anasijisikia amani sana tofauti na alivyokuwa upande wa pili wa Chama cha demokrasia na Maendeleo ( Chadema).
"Nina ladha ya upinzani na ya ccm,kiukweli Chama cha Mapinduzi kinafanya vizuri sana katika kuwatumikia wananchi kwenye kila nyanja,hata mseme nini kiukweli chama hiki lazima kitajwe kila mahali kwa kuwa kimefanya mengi,mfano mzuri ni halmashauri ya mji wa Babati" Paulina Gekul
Gekul ameyazungumza hayo kwenye kikao cha wadau wa Maendeleo katika Halmashauri ya mji wa Babati kilicholenga kupokea maoni na ushauri kuhusu namna ya kuujenga mji huo.
Mpango huo wa kuimarisha uwezo wa Halmashauri za Mji wa Babati katika katika Utoaji wa Huduma unaojulikana kama Urban Local Government Strengthening Programme (ULGSP) Unasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi (OWM-TAMISEMI) na unatekelezwa kupitia Mkopo wa Serikali kutoka Benki ya Dunia (World Bank).
Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi mjini Babati Feisal Hamad ameshauri wakandarasi watakaopewa kazi kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi hiyo wawe wasipewe kwa kujuana.
“Pesa zitakazotolewa na World bank kwa ajili ya maendeleo ya mji wa Babati, zikafanye kazi iliyokusudiwa" alisisitiza Feisal Daudi.
