Mwamuzi Abubakar Mturo amefungiwa miezi mitatu kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo katika mechi iliyochezwa Februari 05, 2020 kati ya Yanga SC v Lipuli FC.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 39(1) ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa Vyombo vya Habari leo imesema kwamba Mturo amefungiwa kosa la kushindwa kumudu mchezo huo ambao Yanga SC iliibuka na ushindi wa 2-1.
Taarifa hiyo inayofuatia kikao cha Februari 10, imeongeza kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 39 (1) ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti wa Waamuzi, ingawa haikuzama ndani kusema kosa lipi refa huyo alifanya siku hiyo.