TMA yatoa tahadhali ya mvua kwa siku tano


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza hali mbaya ya hewa kwa siku tano kuanzia leo.

Taarifa ya TMA imeitaja mikoa inayotarajia kunyesha mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ni mikoa ya Lindi, Mtwara, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Morogoro Kusini pamoja na visiwa vya Unguja, Pemba na Mafia.

Kesho Alhamisi Februari 13, 2020 mvua kubwa itanyesha kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

“Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii,” TMA

Ijumaa ya Februari 14, 2020 angalizo la la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na Kusini mwa mkoa wa Morogoro.

“Upepo mkali na mawimbi makubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba” imeeleza taarifa hiyo ya TMA

TMA imesema Jumamosi ya Februari 15, 2020 angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na Kusini mwa mkoa wa Morogoro