Wachimbaji wadogo wavamia shule wakichimba dhahabu Ushetu



Na Paschal Malulu-Kahama

Imeelezwa kuwa baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika mgodi wa Mwabomba ulioko katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameanza kuvamia eneo la shule ya msingi Mwabomba kwa shughuli za uchimbaji wa madini hayo.

Hayo yameelezwa jana na mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha katika mkutano wa halmashauri kuu chama cha mapinduzi (CCM) kilichofanyika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Kahama amesema serikali imelasimisha baadhi ya maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo lakini wachimbaji hao wameanza kuingia hadi maeneo yasiyoruhusiwa.

Amesema katika shule ya msingi Mwabomba kuna baadhi ya wachimbaji wamevamia maeneo ya shule ambapo ni kinyume cha taratibu za uchimbaji ambapo amewataka wote walioingia katika eneo la shule hiyo kusitisha shughuli za uchimbaji ikiwemo pamoja na kuondoka wasionekane kwani wataanza kukamatwa.

“itafika wakati mwalimu anafundisha darasani halafu pembeni ya madarasa watu wanafanya kazi za uchimbaji kwahiyo tumezielekeza serikali za vijiji na vitongoji kuwaondoa watu hao hakuna kutoa sababu za mkondo wa dhahabu unaelekea huko elimu ni ya muhimu sana kwa watoto ikishindikana tutaufunga mgodi huo”.

Hata hivyo Anamringi Macha ameongeza kuwa kuna baadhi ya migodi ya wachimbaji wadogo imebainika kulima bangi katika maeneo yao hali ambayo kamati ya ulinzi na usalama haitaivumilia na itahakikisha viongozi wa migodi hiyo wanakamatwa ikiwemo kuifunga migodi kuendelea na shughuli za uchimbaji.

Amesema kuna baadhi ya migodi ambayo kamati ya ulinzi na usalama ilifanya ukaguzi ilibaini kulimwa kwa bangi kwa wingi ambacho ni kiashiria tosha kuwa uvutaji wa bangi katika maeneo ya migodi midogo inavutwa hivyo kamati hiyo itaendelea kufuatilia kwa ukaribu ili kuteketeza kilimo cha bangi migodini ikiwemo kuifunga kufanya shughuli za uchimbaji madini.

Aidha kamati kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) wilayani Kahama imekutana kwa ajili ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka minne.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia