F Mvua yafyeka vyumba vinne vya madarasa na ofisi ya walimu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mvua yafyeka vyumba vinne vya madarasa na ofisi ya walimu

Mvua ambayo imefatana na  upepo mkali imebomoa  vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja ya walimu  katika shule mpya ya Sekondari ya Rwandakiseru iliyopo Rorya mkoani Mara.

 Majengo hayo ya shule mpya yamegharimu takribani milioni 35 ikiwa ni pamoja na nguvu ya wananchi ,serikali pamoja na wadau mbalimbali iliyopo kijiji cha Rwandakiseru kata ya Kirongo wilayani Rorya.

Akizungumza na wananchi katika tukio hilo  mkuu wa wilaya ya Rorya Simon Chacha amewataka wananchi kuwa wavumilivu kwa wakati huu mgumu huku akisema kuwa serikali itashirikiana nao  bega kwa bega na ili kuona jinsi gani ya kusaidia ujenzi wa shule hiyo na  upatikanaji wa huduma ya elimu katika kijiji hicho.


Pia mbunge wa wilaya hiyo Lameck Airo amefika katika tukio hilo nakuwapa pole wananchi huku  kukuwasihi wasikate tamaa pia kutohusisha tatizo hilo na ushirikina.

"Tunajua shule hii ilitakiwa kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza siku nne zijazo na imeharibiwa na upepo msihusishe tukio hili na ushirikina " ,Alisema Airo.


Aidha mmoja wa wananchi walioshiriki ujenzi wa shule hiyo Everine Daniel amesema kuwa wamesikitishwa na tukio hilo kwani wanafunzi wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwenda  shule ya Sekondari kirogo suala ambalo lilikuwa likipelekea kumka saa kumi usiku ili kuwahi masomo nakuiomba serikali kuwasaidia wanafunzi hao ambao wamepangiwa kujiunga na shule hiyo  kujiunga na shule hiyo wakati wananchi na wadau mbalimbali wakiendelea na jitihada za ukarabati wa majengo hayo.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kirunga Vitalis Joseph amempongeza mkuu wa wilaya ya Rorya Simon  Chacha pamoja na mbunge wa wilaya hiyo Lameck Airo kwa kuungana na wananchi wakati huu mgumu na kuwaomba kufanyia kzi maombi ya wananchi katika kuhakikisha wanatatua tatizo hilo kupitia wadau mbalimbali , wananchi pamoja na serikali.