Waziri Mkuu wa Lesotho ashinikizwa kujiuzulu


Shinikizo la kumtaka Waziri Mkuu wa Lesotho Thomas Thabane ajiuzulu limezidi kuongezeka hapo jana, baada ya kusimama mbele ya mahakama kwa madai ya kumuua mke wake kabla ya kumuoa mkewe wa sasa.

Mahakama hiyo ya huko Maseru ilitarajiwa kumsomea mashtaka Thabane kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ya Lipolelo Thabane, yaliyotokea Juni mwaka 2017 akiwa na umri wa miaka 58.

Lakini baada ya kikao kifupi, suala hilo limeamuliwa kuwasilishwa katika Mahakama Kuu na waziri mkuu huyo hakushtakiwa rasmi.

Tarehe pia haikuwekwa wazi, ambapo waziri mkuu huyo atatakiwa kufika mbele ya Mhakama Kuu.

Kamati ya utendaji ya chama chake cha All Basotho Convention (ABC) imemtaka ajiuzulu mara moja, huku ikitafuta kiongozi wa kuchukua nafasi yake. Wakati wa mauaji hayo, Thabane alikuwa katika mchakato wa kumpa talaka Lipolelo.