Coronavirus: Mahakama kuu Zanzibar yasitisha usikilizaji wa kesi kwa siku 30

Na Thabit Madai,Zanzibar.



MAHAKAMA Kuu Zanzibar imesitisha  usikilizwaji wa kesi zote kwa muda wa siku 30 kuanzia March 26 hadi Aprili 24 kutokana na kuchukua  tahadhari za  kujikinga  maambukizi ya virusi vya corona (covid-19).

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Vuga Mjini Unguja, Mrajisi wa Mahakama kuu Zanzibar, Mohamed Ali Mohamed amesema kwamba wamefikia uwamuzi huo kutokana na maagizo yaliyotolewa na Serikali mnamo tarehe 17 March mwaka huu juu ya kujikinga na kuenea kwa virusi vya Corona (COVID- 19).

Alisema usititishwaji wa kusikiliza kesi kwa muda wote wa siku 30 ni kwa mahakama zote kutokana na kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.



“Kuanzia leo March 26 kutasitishwa usikilizwaji wa kesi kwa muda wa siku 30, kwa zile kesi ambzo zipo hatua ya kusikiliza ‘Submisition’,Mahakama itawashauri Mawakili au wenye kesi kuwasilisha kwa njia ya maandishi” alisema Mrajisi huyo.



Pia alisema  kwa kipindi hicho Mahakama zitashughulikia kesi za dharura na kwa washtakiwa wenye kesi nzito na maombi ya dhamana  hivyo muombaji na wakili wake au wadhamini ndio watakaruhusiwa kuingia Mahakamani.



“Kwa Makosa yenye dhamana, Majaji na Mahakimu wanatakiwa kutoa dhamana yenye masharti nafuu ili kupunguza mrundikano wa katika Chuo  cha Mafunzo (Magereza) kwa kipindi hichi cha mripuko wa mripoko wa virusi vya Corona” alisema Mrajisi huyo.



Aidha alisema katika kipindi hichi watendaji wote wa Mahakama wataendelea kuwepo kazini hivyo kumbi za Mahakama (Open Court) hazitatumika.



“Kwa Majaji na mahakimu wenye hukumu na maamuzi (Ruling) watatumi kipindi hichi katika kuzikamilisha” alieleza Mrajii huyo.



Hadi sasa Zanzibar imeripoti visa vya wagonjwa wawii ambao wamebukizwa virusi ambapo wanaendelea vizuri na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua hatua kadhaa za kujikinga na miripuko wa virusi hivyo.