TAMWA yatao ushauri kwa wazazi na walezi kuhusu kujikinga na virusi vya Corona

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimewashauri Wazazi, Walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha kuwa watoto wanabaki ndani katika kipindi hichi ambacho shule na madrasa zikiwa zimefungwa.

Ushauri  huo umetolewa na Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar, Dk  Mzuri Issa  katika taarifa yake aliyoitoa leo kwa  vyombo mbali mbali  vya Habari nchini.

Dk Mzuri alisema kwamba Zanzibar ikiwa ni sehemu ya dunia imefunga mikusanyiko yote kama njia mojawapo ya kupambana na maradhi yanayosababishwa na virusi vya Corona au  COVID-19 hivyo ni vyema kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wanakuwa ndani kama njia salama ya kuwaepusha na maambukizi ya virusi hivyo.

Alieleza kuwa katika maeneo mbali mbali bado watoto wanaonekana wakicheza nje kwa vikundi jambo ambalo linaweza kupelekea maambukizi ya maradhi haya hatari.

“Muhimu wazee kuhakikisha kuwa watoto wanabaki ndani wanajisomea na kufanya shughuli nyengine chini ya uangalizi makini,” alisema Dk Mzuri.

Aidha aliwaomba  Wazee pia kuwaelimisha watoto mfululizo  sababu ya kuzuiwa kutokwenda skuli na madrasa kwamba wabakie ndani na siyo kuzurura nje.

Alongeza kusema kuwa  hali hii itaweza kuwalinda dhidi ya maradhi haya mabaya ya kuambukiza kwa aina tofauti ikiwemo kushika sehemu hiyo hiyo ambayo mwenye maambukizi ameshika.

“Kubakia ndani chini ya uangalizi maalum pia kutawalinda dhidi ya watu wabaya ambao wakati mwingi hutumia nafasi wanayoipata na kuwafanyia vitendo viovu watoto ikiwemo kuwabaka.”alisema Dk Mzuri Issa.

Katika hatua nyingine Dk Mzuri aliwapa pole wanajamii, Serikali na dunia kwa jumla kwa kupitia katika kipindi hichi kigumu cha maradhi ya COVID-19 ambayo yanaendelea kuyatesa mataifa mengi ulimwenguni.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items