Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, Jaji Semistocles Kaijage amesema tume hiyo imekamilisha awamu ya kwanza ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura nchi nzima sambamba na kuanza kutoa taarifa za wapiga kura walioandikishwa.
Jumla ya wapiga kura waliopo katika Daftari la awali kwa sasa ni milioni thelathini laki moja themanini na saba elfu mia tisa na themnanini na saba, idadi hiyo inawez kubadilika kutokana na uhakiki wa uchakataji wa taarifa za wapiga kura endapo watabainika waliojiandikisha zaidi ya mara moja.
Akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa viongozi wa vyama vya siasa nchini, Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa pamoja na mafanikio ya uandikishaji wa daftari la wapiga kura na mwitikio mkubwa wa wapiga kura tume hiyo ilikutana na changamoto kadhaa katika kipindi hicho cha uboreshaji ikiwemo uharibifu wa miundombinu katika baadhi ya maeneo hivyo watendaji wake kushindwa kufika kwa wakati katika maeneo ya uandikishaji.
Changamoto nyingine ni baadhi ya wananchi kutozitumia vyema siku saba zilizopangwa kwa ajili ya uandikishaji na kujikuta wanajitokeza siku za mwisho na hivyo kusababisha msongamano mkiubwa siku ya mwisho.
Aidha amesema taarifa za daftari la awali zitabandikwa kwenye kila kituo ambapo amebainisha vituo vilivyopo ni elfu nane kabla ya kuanza uhakiki wa daftari hilo kwa awamu ya pili.
Awamu ya pili zoezi la uandikishaji wapiga kura litawahusu wapiga kura ambao taarifa zao hazikuwemo katika daftar la awamu ya kwanza sambamba na wale ambao hawakuwemo nchini.