Umoja wa Ulaya kutafuta mpango wa pamoja kuhusu virusi vya corona

Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanajaribu kutafuta msimamo wa pamoja katika kushughulikia madhara ya maradhi ya COVID-19 ambayo yamelemaza uchumi wa nchi wanachama.

Italia na Ufaransa zinapendekeza kuwepo mshikamano katika kuchochea ukuaji wa uchumi. Hadi sasa kila nchi imekuwa ikichukua hatua peke yake, baadhi zikifunga mipaka yao na kukwamisha usafiri wa mahitaji muhimu yakiwemo ya kimatibabu, na kukiuka vikomo vya matumizi vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya.

Rais wa Halmashauri Kuu ya umoja huo Ursula von der Leyen, amesema wakati nchi wanachama zilipohitaji zaidi kusaidiana, kila moja iliweka mbele maslahi yake.

Von der Leyen amesema anataka kuweka mpango wa pamoja wa Ulaya wa kutafuta suluhu kwa athari za COVID-19, ambao utajadiliwa na wakuu wa nchi za Ulaya katika mkutano utakaoandaliwa kwa njia ya video.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia