Bongia mashuhuri nchini Australia Wilhelm Ott abadili dini na kuwa muislamu baada ya kuvutiwa na mwenendo wa rafki yake mturuki.
Wilhelm Ott , bondia nchini Australia abadili dini na kuwa muislamu baada ya kuvutiwa na mwenendo wa rafiki yake mturuki .
Bondia huyo ameonekana katika video akitoa shahada, ishara kuwa anakubali na kuamini uislamu amesema kuwa anamshukuru Allah kumonesha imani ya haki.
Wilhelm Ott amesema kuwa kuwa muislamu ilikuwa malngo yake ila alikuwa bado hajakinahi kutokana na taarifa nyingi ambazo zilikuwa zikimchanganya kutokana na uislamu anavyozungumziwa, ila katika kipindi cha agizo la kutotoka ndani kutokana na virusi vya corona ameweza kujifunza mengi na kupata nguvu ya kuchukuwa uamuzi wa kuwa muislamu.
Wilhelm Ott ana umri wa miaka 37.
Katika video yake hiyo, Wilhelm Ott amesema kwamba rafiki yake mturuki pia umemsaidia na kumpa Quran yake ya kwanza.
