China yaripoti kesi mpya saba za wagonjwa wa corona


Mkoa wa Kaskazini Magharibi wa China wa Shaanxi umeripoti leo Jumamosi kesi saba mpya za wagonjwa wa Corona ambao ni Raia wa China walioingia nchini humo wakitokea nchini Urusi.

Jiji la bandari la Manzhouli huko Inner Mongolia pia liliripoti kesi mpya tatu za wagonjwa wa Corona.

China ilianzisha ukaguzi mkali mnamo Machi 28 katika bandari zake na maeneo ya mipaka, na kupiga marufuku kuingia kwa raia wa kigeni.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items